Print this page

Marekani mwenyeji mashindano ya Fomula 1

Las vegas, Marekani
Mashindano ya Formula 1 yanaelekea nchini Marekani wikiendi hii kwa ajili ya US Grand Prix huko Austin, Texas, tukio ambalo limekuwa kipenzi kikubwa katika kalenda ya mashindano hayo tangu mbio za kwanza kufanyika hapo mwaka 2012.
Austin ni mojawapo ya matukio matatu ya F1 yatakayofanyika nchini Marekani; Miami ikiandaa mashindano mwezi Mei na Las Vegas ikiandaa mbio za usiku mwezi Novemba.
Umaarufu wa mchezo huu nchini Marekani umekua katika miaka ya hivi karibuni, jambo lililochangiwa kwa kiasi kikubwa na mfululizo wa vipindi vya ‘Drive to Survive’ vinavyooneshwa kwenye Netflix.
Hata hivyo, ni wazi kuwa uhusiano kati ya F1 na Marekani umekuwa wa kupanda na kushuka kwa miaka mingi na baadhi ya mashindano yalifanikiwa sana na kukumbukwa kwa furaha, huku mengine yakiwa hayakuwa na mafanikio makubwa kiasi hicho.
Shirika la F1 liliazimia kufanikisha tukio hili kiasi kwamba liliwekeza dola milioni 500 kununua eneo la ardhi, ambapo lilijenga jengo jipya la huduma za magari (pit building) na eneo la maandalizi (paddock). 
Aidha, Las Vegas ina mkataba wa muda mrefu wa kuandaa mbio za F1, angalau hadi mwaka 2037, huku mbio za mwaka huu zikipangwa kufanyika mwezi Novemba.

Rate this item
(0 votes)
Japhet