DAR ES SALAAM
Na Remigius Mmavele
Rigobert Bamundele Ifoli, maarufu kwa jina Rigo Star, alizaliwa Agosti 28,1955 jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).Rigo Star ni mpiga gita hodari aliyetikiza duniani kwa kupiga chombo hicho, alianza kuonyesha uwezo wake akiwa na umri mdogo ambapo alikuwa mmoja wa wapiga gitaa wenye ushawishi mkubwa nchini mwake.