Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu awageukia Viongozi Halmashauri ya Walei

Paroko mpya wa Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia - Goba Mwisho, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Festo Liheta akishika funguo za Kanisa, baada ya kusimikwa kuwa paroko, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyofanyika Parokiani hapo. Nyuma ya Paroko ni Makatekista na Viongozi wa Halmashauri ya Walei Paroko mpya wa Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia - Goba Mwisho, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Festo Liheta akishika funguo za Kanisa, baada ya kusimikwa kuwa paroko, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyofanyika Parokiani hapo. Nyuma ya Paroko ni Makatekista na Viongozi wa Halmashauri ya Walei

Dar es Salaam

Na Mwandishi wetu

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, amewataka Viongozi wa Halmashauri ya Walei, wanaochaguliwa ngazi mbalimbali za Kanisa Katoliki, kufanya kazi za kitume na sio kuleta majungu, umbea na kuchonganisha Mapadri.
Wito huo aliutoa wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia - Goba Mwisho, iliyokwenda sambamba na kumsimika Paroko mpya wa Parokia hiyo Padri Festo Liheta.
Askofu Mchamungu alisema kuwa viongozi wengi wa Halmashauri ya Walei, huwa wanasahau majukumu yao waliyochaguliwa katika kazi ya Kanisa, bali utakuta wanafanya kazi za Paroko au Paroko msaidizi na kuwamiliki Makasisi hao, “Msifanye hivyo viongozi, bali fanyeni kazi mlizochaguliwa na Waamini, acheni malumbano kila wakati na Mapadri.”

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.