DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo amewataka Wajumbe wa Kamati ya Huduma ya Mikopo ngazi ya Kata, kuhakikisha wanakuwa vinara wa ukusanyaji marejesho ya Mkopo huo wa asilimia 10.
Mpogolo alisema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza katika hafla ya uapisho wa uwajibikaji na uadilifu katika utoaji na usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 kwa wajumbe wa kamati hiyo.