HISTORIA YA KANISA
Na Askofu Mstaafu Method Kilaini
Mitume na wafuasi wa Kristo toka mwanzo kilele na kitovu cha Imani yao kilikuwa kifo na ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo. Injili zote zinasimulia juu ya wiki ya mwisho ya maisha ya Bwana wetu Yesu Kristo ulimenguni au kwa naneno mengine tunachoadhimisha kama Juma Kuu ikiwa ni matukio ya kuwaaga mitume, kushikwa, kufa na kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Hiki ndicho kilikuwa kilele cha simulizi zote. Kwa namna ya pekee tunayakuta katika Injili ya Mt. Yohana sura ya 12 hadi 20, ambayo inasimulia kwa kinaganaga juma hilo kuu. Mtakatifu Yohana alikuwa shuhuha wa matukio haya yote na hadi kifo chake aliyakumbuka kwa uwazi, yalimwachia alama kubwa katika maisha yake.
Yesu Kristo alikufa na kufufuka wakati wa maadhimisho ya Pasaka ya Wayahudi. Katika siku hizo Wayahudi humkumbuka Musa na kukombolewa kwao kutoka utumwani Misri. Huadhimisha mapatano kati ya Mungu na taifa lao la Israel.
Pasaka, yalikuwa ni maadhimisho ya juma zima, wakikumbuka na kusimilia historia yao kuanzia baba zao walipokula chakula cha mwisho huko Misri, ikiwa ni mkate bila kutiwa chachu na mboga chungu na nyama ya kondoo, ambaye damu yake waliipaka milango yao.
SOMA ZAIDI KATIKA TUMAINI LETU.