DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam amewataka Waamini kumtangaza Kristo, aliyefufuka kutoka kwa wafu.
Kardinali Pengo aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Pasaka, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Benedicto Abate-Wazo Hill.
“Katika kumtangaza Kristo inatakiwa uwe tofauti na wengine kwa sababu wewe umepata Sakramenti, na uwe na msimamo wa kiimani na siyo kusema tu kwa sababu ni
maneno ambayo umeambiwa au kuhadithiwa, bali aone katika maisha yako kwamba una imani hiyo iliyo thabiti,”alisema Kardinali Pengo.
Kardinali Pengo alisema kwamba Kristo alimuita kila mmoja kudhihirisha ufufuko wake katika maisha ya kila mtu, na hiyo ndio iliwaongoza wafuasi wa Bwana tangu mwanzo wake na wote walikubali kufa kwa sababu hiyo.