Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kard. Pengo ataka Waamini kumtangaza Yesu Kristo

Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Augostino, Salasala, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Pasaka. (Picha na Yohana Kasosi) Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Augostino, Salasala, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Pasaka. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam amewataka Waamini kumtangaza Kristo, aliyefufuka kutoka kwa wafu.
Kardinali Pengo aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Pasaka, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Benedicto Abate-Wazo Hill.
“Katika kumtangaza Kristo inatakiwa uwe tofauti  na wengine kwa sababu wewe umepata Sakramenti, na uwe na msimamo wa kiimani na siyo kusema tu kwa sababu ni

maneno ambayo umeambiwa au kuhadithiwa, bali aone katika maisha yako kwamba una imani hiyo iliyo thabiti,”alisema Kardinali Pengo.
Kardinali Pengo alisema kwamba Kristo alimuita kila mmoja kudhihirisha ufufuko wake katika maisha ya kila mtu, na hiyo ndio iliwaongoza wafuasi wa Bwana tangu mwanzo wake na wote walikubali kufa kwa sababu hiyo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.