Mtwara
Na Mwandishi wetu
Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Mhashamu Michael Msonganzila amewataka wanawake kuwa wanyenyekevu kama Mama Bikira Maria.
Alisema hayo wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 40 ya Parokia, na Miaka 20 ya Utume wa Padri Fintani Mrope, Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme, Tandahimba Jimbo Katoliki la Mtwara, iliyofanyika parokiani hapo.
Askofu Msonganzila alisema kwamba Waamini wengi wanayumbayumba kila sehemu katika imani, hiyo yote ni kutangatanga bila kuelewa wanachokitafuta.