Dar es Salaam
Na Mathayo Kijazi
Waandishi wa Habari wametakiwa kuwa wabunifu na wenye kujitolea kufanya vitu vya tofauti katika kazi zao, ili waweze kuzalisha vipindi na habari zenye ubora.
Hayo yalisemwa na Derik Murusuri, Mwezeshaji katika Semina ya Waandishi wa Habari, iliyofanyika hivi karibuni Msimbazi Centre, jijini Dar es Salaam.