Ahadi ya serikali ya kufikisha umeme wa gridi ya taifa katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera, imetekelezwa baada ya kusaini mikataba ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220, kutoka Benako-Ngara hadi Kyaka wilayani Misenyi.
Aidha, hatua hiyo imekwenda sanjari na kituo cha kupoza umeme cha Benako cha msongo wa kilovoti 220/33, na kutoa uhakika kwa Mkoa huo kupata umeme wa gridi na kuacha kutegemea umeme kutoka Uganda.