Morogoro
Na Angela Kibwana
Kanisa Katoliki limehitimisha mfungo maalumu kote nchini, ambapo Wakatoliki walifunga, kuabudu Ekaristi Takatifu na kuiombea nchi haki na amani, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Hatua ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), kutoa sala maalumu na agizo la kuwashirikisha Waamini kufunga, kusali na kuombea haki na amani si mara ya kwanza, bali limefanya hivyo mara kwa mara hasa inapoonekana kuna viashiria vya uvunjifu wa amani, ambayo ni tunda la haki.