Dar es Salaam
Na Mathayo Kijazi
Wakristo wametakiwa kuwa na misalaba katika nyumba zao, iwasaidie kumshinda shetani pale anapowakaribia.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, alitoa siri hiyo hivi karibuni wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyokwenda sanjari na utoaji wa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa vijana 52, katika Parokia ya Mtakatifu Maurus - Kurasini, jijini Dar es Salaam.