Print this page

Serikali yadumisha huduma kwa wazee

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Wakili Amon Mpanju, akisalimiana na Wazee wakati wa ziara yake katika makazi ya Wazee wasiojiweza, yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Wakili Amon Mpanju, akisalimiana na Wazee wakati wa ziara yake katika makazi ya Wazee wasiojiweza, yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida.

Manyoni

Na Jackline Minja

Katika kuelekea kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, serikali imeendelea kudumisha huduma bora kwa wazee, kwa kuhakikisha kundi hilo linapata huduma za msingi, zinazowawezesha kuishi maisha yenye heshima, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
 Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Wakili Amon Mpanju, wakati wa ziara yake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza, yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida.

Rate this item
(0 votes)
Japhet