Tabora
Na Mwandishi wetu
Kauli ya Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference: TEC), Mhashamu Wolfang Pisa, ya kuwataka Wakatoliki kulinda usafi wa Kanisa, na kutokubali Kanisa hilo linajisiwe na kudhoofishwa, bado imeendelea kutikisa kila kona.
Askofu Pisa, ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, alitoa kauli hiyo yenye kuvuta na kugusa hisia za wengi hivi karibuni, wakati alipokuwa akitoa homilia yake, katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 100, ya Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo - Kipalapala, Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.