Dar es Salaam
Na Mathayo Kijazi
Dekano wa Dekania ya Mavurunza, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Vivian Menezes- OCD, amewasihi Waamini kufahamu kwamba kuwa na mali nyingi kusiwe sababu ya wao kufarakana na Mungu, kwani kila walichonacho kinatoka kwake.
Padri Vivian alisema hayo wakati wa homilia yake, alipomwakilisha Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, kuadhimisha Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa vijana 119, katika Parokia ya Mtakatifu Yohane Maria Muzeey - Tegeta ‘A’.