Morogoro
Na Mwandishi wetu
Imeelezwa kwamba Ndoa Takatifu ya mume mmoja na mke mmoja, sasa imekuwa kama maigizo.
Padri Ferdinand Mushi, Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Jordan, Jimbo Katoliki la Morogoro, alisema hayo wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu, ya Sakramenti Takatifu ya Ndoa kati ya Bwana Edwin Marandu na Bibi Anna Ndimbo, iliyofanyika Parokia Teule ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu Tungu, Jimboni humo.