Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddeus Ruwa’ichi, amewataka Waamini kutoruhusu kugubikwa na huzuni iliyopitiliza pale msiba unapotokea, badala yake waweke imani na tumaini katika Kristo, liwafariji.
Askofu Mkuu huyo alisema hayo wakati wa homilia yake, katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kumwombea Balozi wa Baba Mtakatifu, Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jimboni humo.