Dar es Salaam
Na Celina Matuja
Wanafunzi wanaohitimu masomo yao ya Sekondari, katika Shule ya Msingi na Sekondari ya St. Rosalia Kinyerezi, jijini Dar es Salaam, wanapaswa kuangalia fursa za kusomea ubaharia, kwani ni taaluma inayoweza kuwasaidia maishani.
Wito huo ulitolewa na CPA Pascal Karomba, Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), wakati akizungumza katika mahafali ya shule hizo, kwa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari, ili wapate elimu hiyo nzuri ya ubaharia.
Aidha, Karomba aliupongeza uongozi wa shule hizo, kwa kuiona kiu ya Watanzania juu ya elimu, kuondoa ujinga kwa watoto wa kitanzania.