Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Wahitimu St. Rosalia waelekezwa Ubaharia

Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Boneventura - Kinyerezi, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Francis Hiza akiwabariki Wahitimu wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari ya St. Rosalia wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani kwa Mahafali kwa wanafunzi hao yaliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo. Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Boneventura - Kinyerezi, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Francis Hiza akiwabariki Wahitimu wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari ya St. Rosalia wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani kwa Mahafali kwa wanafunzi hao yaliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.

Dar es Salaam

Na Celina Matuja

Wanafunzi wanaohitimu masomo yao ya Sekondari, katika Shule ya Msingi na Sekondari ya St. Rosalia Kinyerezi, jijini Dar es Salaam, wanapaswa kuangalia fursa za kusomea ubaharia, kwani ni taaluma inayoweza kuwasaidia maishani.
Wito huo ulitolewa na CPA Pascal Karomba, Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), wakati akizungumza katika mahafali ya shule hizo, kwa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari, ili wapate elimu hiyo nzuri ya ubaharia.
Aidha, Karomba aliupongeza uongozi wa shule hizo, kwa kuiona kiu ya Watanzania juu ya elimu, kuondoa ujinga kwa watoto wa kitanzania.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.