DAR ES SALAAM
Na Shemasi George Timalias
Karibu ndugu msikilizaji wa Radio Vatican, katika tafakari hii, inayotugusa kwa karibu sana, ambayo inakumbusha Sikukuu ya Watakatifu wote, kila ifikapo tarehe Mosi Novemba ya kila mwaka, lakini pamoja na Watakatifu, kuna ndugu zetu Marehemu wote waliotutangulia mbele ya haki, ambapo Mama Kanisa anatupatia fursa ya kuwakumbuka, kila ifikapo tarehe 2 ya mwezi Novemba na kuendelea hadi mwisho wa mwezi.
Kwa hiyo tuanze tafakari hii, sehemu ya kwanza ya Watakatifu. Fundisho kuu tunalopata katika siku hii ya watakatifu wote, ni msisitizo wa maisha yetu kuishia mikononi mwa Mungu aliyetuumba huko mbinguni.