Bagamoyo
Na Mathayo Kijazi
Wakristo wametakiwa kuepuka kiburi na majivuno, kwa kudhani bila wao mambo hayawezi kufanyika katika Kanisa, na jamii kwa ujumla.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Musomba -OSA, wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, sanjari na kutoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, katika Parokia ya Mtakatifu Toma – Muungano, jimboni humo.
“Tunaona katika Injili ya leo, yule Farisayo anamwambia Mungu ‘Mbona huoni? Mimi niko moja, mbili, tatu, mimi nafanya hiki na hiki, siwezi kuwa kama huyo, huyo ni mdhambi, huyo anatoza ushuru. Kwa hiyo anaona kwamba yeye ni bora kuliko yule mwingine. Na ndio maana kwa kuigaiga, tunaweza kusahau njia yetu ya kumwelekea Mungu.