Kagera
Na Silivia Amandius
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Wakili Amon Mpanju, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii mkoani Kagera, kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wengine, ili kuwaleta wananchi pamoja.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki, kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii katika Mkoa wa Kagera, Mpanju alisema kuwa maendeleo ya kweli yapo kwa wananchi, hivyo ni muhimu watumishi hao kuwafikia hadi ngazi za vijiji.