Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, amewataka Waamini kumshukuru Mungu kwa kila jambo, kwani yeye ndiye muweza wa yote.
Askofu Mchamungu alitoa wito huo katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyokwenda sanjari na kutoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara Kwa vijana 31, iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Yohane Paulo II, Miembesaba-Kibaha jimboni humo.