Dar es Salaam
Na Mwandishi wetu
Paroko Msaidizi wa Paroki ya Mtakatifu Rita wa Kashia -Goba, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Kanuti Martin Nyoni, amewataka Waamini waendelee kusali na kumuomba Mwenyezi Mungu, ili Taifa liendelee kuwa na viongozi waadilifu, wenye kusikia sauti yake Mwenyezi Mungu, katika kuwalinda na kuwaongoza raia.
Padri Nyoni alitoa wito huo hivi karibuni, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu, ya kuwaombea Watu wote waliouawa na kujeruhiwa, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu iliyofanyika parokiani hapo.