VATICAN CITY, Vatican
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni, Baba Mtakatifu Leo XIV, amekazia kuhusu furaha ya Mama Kanisa kwa zawadi ya Bikira Maria aliyekingiwa dhambi ya asili, kielelezo cha usafi na utakatifu, ili aweze kumzaa Kristo Yesu, Mwana wa Mungu kwa ajili ya wokovu wa walimwengu, Sherehe ambayo ilitangazwa Desemba 8, 1854 na Papa Pio IX.
Papa aliyasema hayo katika Maadhimisho ya Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, sherehe ambayo ilitangazwa Desemba 8, 1854 na Papa Pio IX.