Dar es Salaam
Na Mathayo Kijazi
Imeelezwa kuwa kila anayepokea Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, anatumwa kuwa Mkristo kweli aliye tayari kuacha dhambi na kumrudia Mungu, huku akiwa mtu wa toba.
Hayo yalisemwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana 72, katika Parokia ya Mtakatifu Maria Magdalena – Kimara Mtoni, jimboni humo.