Kisarawe – Pwani
Na Mathayo Kijazi
Chansela wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Vincent Mpwaji, amewaalika Wakristo kutafakari na kutambua kwamba jukumu lao la kwanza la msingi, ni kuwa Mashahidi wa Yesu Kristo.
Padri Mpwaji aliyasema hayo katika homilia yake, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana 21, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph Cottolengo – Masaki - Kisarawe, jimboni humo.