Katika safu hii ya Chimba Chimba Historia ya Kanisa wiki iliyopita, tuliendelea kuwaletea historia ya mitaguso mikuu, kwa kuendelea na Mtaguso Mkuu wa Kostantinopole. Leo tunawaletea historia ya kuasi kwa Kanisa la Wakopti Misri, na historia ya Mababa wa Kanisa wa Magharibi. Sasa endelea…
Bahati mbaya, Wakristo wa Misri ambao kabla walikuwa kila mara wanashinda, na hivyo wakajiona kama watetezi imara wa imani, mara hii waliposhindwa hawakufurahi. Walishinda wakati wa Arius na walishinda wakati wa Nestorius, lakini sasa kwa kusisitiza mno umoja na umungu wa Kristo walishindwa.
Hawakupokea kushindwa, hivyo Kanisa zima likaendelea na uzushi huo ulioitwa ‘Monophysitism’, maana yake Yesu ni Mungu na utu wake umekandamizwa.