Dar es Salaam
Na Joseph Mihangwa
Chimbuko la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyofanyika Visiwani humo Januari 12, 1964.
Bila Mapinduzi hayo tusingezaliwa Tanzania, wala Chama tawala cha sasa - Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho ni Muungano wa Vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanganyika, na Afro-Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar.
Chama kilichozaliwa Februari 5, 1977, miaka 13 baada ya Muungano uliofikiwa Aprili 26, 1977, ni matokeo ya kero za Muungano.
Mapinduzi haya yaliyoshangaza dunia kwa staili yake, yalifanyika kwa harakati za siasa za mrengo wa Kikomunisti, na kutia hofu nchi za Magharibi, hasa Marekani na Uingereza, zikaamua kuingilia kati kuyadhibiti Mapinduzi hayo, kuzuia kuenea kwa Ukomunisti Afrika kupitia Afrika Mashariki.