MWANZA
Na Paul Mabuga
Hebu vuta picha: Zamani kijana wa Kitanzania hakukurupuka tu kuitwa mzazi. Kulikuwa na mifumo madhubuti ya Jando, Unyago, na yale mafunzo ya kando ya moto kutoka kwa babu na bibi, yaliyomjenga mtu kifikra na kihisia.
Lakini leo, “moto” pekee unaowaunguza vijana wetu ni wa data za simu, na mianga ya mitandao ya kijamii. Wakati mifumo hiyo ya kijadi ikipumzika kwenye makaburi ya historia, tunapaswa kujiuliza kwa uchungu: Je, vijana wetu wanajifunza wapi kuwa wazazi?