Dar es Salaam
Na Laura Mwakalunde
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amesema kuwa haki na amani ni vitu viwili vinavyotegemeana, na haviwezi kutenganishwa.
Askofu Mkuu Ruwa’ichi alisema hayo hivi karibuni, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Mkesha wa Noeli, uliofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Yosefu, jimboni humo.
“Amani na haki ni zawadi na ni wasifu unaofungamana na Kristo Mwokozi, kwani Watanzania wengi kwa ujinga na kurubuniwa, wanajidai wao ni wadau wa amani na kusahau kuwa, hakuwezi kuwa na amani bila haki,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.