Gairo
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Japhari Kubecha, ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilayani humo kwa kazi nzuri ya ukusanyaji mapato ya serikali.
Aidha amesisitiza kwamba juhudi hizo zimechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa rasilimali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akizungumza ofisini kwake baada ya kutembelewa na Meneja wa TRA Wilaya ya Gairo, Ditram Wila, pamoja na Afisa Mwandamizi Elimu na Mawasiliano wa TRA Mkoa wa Morogoro, Immaculate Chaggu, waliofika kumpatia zawadi ya Ushirikiano wa mwaka 2025 kutokana na mshikamano aliouonyesha kwa mamlaka hiyo, DC Kubecha alisema TRA imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wafanyabiashara wanatimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati.
Aidha, alieleza kuwa ushirikiano mzuri kati ya TRA, wafanyabiashara na viongozi wa serikali ni msingi muhimu wa mafanikio katika ukusanyaji wa mapato.