Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

DC ahimiza ukusanyaji maduhuli ya Serikali

Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Japhari Kubecha akizungumza na Meneja wa TRA Wilaya ya Gairo, Ditram Wila na Afisa Mwandamizi Elimu na Mawasiliano wa TRA Mkoa wa Morogoro, Immaculate Chaggu walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni. Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Japhari Kubecha akizungumza na Meneja wa TRA Wilaya ya Gairo, Ditram Wila na Afisa Mwandamizi Elimu na Mawasiliano wa TRA Mkoa wa Morogoro, Immaculate Chaggu walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni.

Gairo

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Japhari Kubecha, ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilayani humo kwa kazi nzuri ya ukusanyaji mapato ya serikali.
Aidha amesisitiza kwamba juhudi hizo zimechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa rasilimali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akizungumza ofisini kwake baada ya kutembelewa na Meneja wa TRA Wilaya ya Gairo, Ditram Wila, pamoja na Afisa Mwandamizi Elimu na Mawasiliano wa TRA Mkoa wa Morogoro, Immaculate Chaggu, waliofika kumpatia zawadi ya Ushirikiano wa mwaka 2025 kutokana na mshikamano aliouonyesha kwa mamlaka hiyo, DC Kubecha alisema TRA imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wafanyabiashara wanatimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati.
Aidha, alieleza kuwa ushirikiano mzuri kati ya TRA, wafanyabiashara na viongozi wa serikali ni msingi muhimu wa mafanikio katika ukusanyaji wa mapato.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.