DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu
Kufuatia timu ya taifa, Taifa Stars, kuondoshwa katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), Watanzania wengi ambao ni mashabiki wa soka, wameamua kuzivamia kurasa za mitandao ya kijamii, zilizo chini ya Shirikisho la soka Afrika CAF, na kurusha maneno makali.
Stars iliondoshwa mashindanoni Januari 4 mwaka huu, kwa kuchapwa na Morocco bao 1-0, huku mwamuzi Boubou Traore kutoka nchini Mali, akionekana kuinyonga Tanzania kupitia maamuzi yake mabovu, ikiwemo kunyimwa haki ya kupiga pigo la penati, katika dakika za mwisho za mchezo.