Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Nyboma Njia ngumu ya kufanikisha safari yake ya muziki

DAR ES SALAAM

Na Remigius Mmavele

Nyboma Mwan’dido Danos David Laurent Canta, alizaliwa Desemba 24, 1952 katika mji wa Nioki uliopo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mkongwe huyu wa muziki aliyeanza muziki akiwa na umri wa miaka 18, amejizolea sifa ulimwenguni kote kutokana na sauti yake ya dhahabu.
Alianza muziki mwaka 1969 alipojiunga na bendi ya Baby National iliyokuwa inaongozwa na Freddy Mulongo. Akiwa katika bendi hiyo, Nyboma alipata fursa ya kutunga wimbo wake wa kwanza unaoitwa ‘Apolosa.Baada ya hapo alijiunga na bendi inayoitwa wa Super Mosinzo.
Akiwa katika bendi hiyo, Nyboma alipata wadhamini wawili, ambao ni Achille Ngoy ambaye alikuwa Mkurugenzi anayehusika na sanaa kwenye Gazeti la Likembe. Mdhamini mwingine ni Bavon Marie-Marie, mdogo wake Franco Luambo.
Bavon Marie-Marie alikuwa na matumaini makubwa kwa Nyboma kwa kuwa alikuwa na fikra ya kuanzisha bendi yake aliyotaka iitwe  ‘Bana 15 Ans’ bendi ambayo alikuwa na kusudio la kumchukua Nyboma kuwa mwimbaji wake kinara.
Isivyo bahati, Bavon Marie-Marie akafariki ghafla, kifo kutokana na ajali ya gari aliyokuwa akiendesha, na huo ndio ukawa mwisho mipango yake yote, na marehemu Bavon. Akiwa bado Mtu ambae anajitafuta, Nyboma alijiunga na kundi la Negro Succès ambako ndiko alikoanza kujiimarisha zaidi kimuziki.
Mwaka 1970, baada ya kifo cha Bavon ambaye alikuwa kiongozi mwenza wa kundi la Negro Succes, Nyboma aliondoka kwenye kundi hilo, na mwaka 1972 akajiunga na kundi la “Bella-Bella” lililokuwa linaongozwa na wanandugu wawili  Maxime na Emile Soki lililokuwa chini ya lebo ya Verckys’s.
Akiwa katika kundi hilo, alitunga nyimbo LILI, PETE TOSI TOLATA, MBUTA. Wimbo Mbuta ndio uliotokea kupendwa na wapenzi wengi wa muziki. Katika wimbo huo, Nyboma ameshirikiana na Pepe Kalle.
Baada ya muda, ukatokea mtafaruku kati ya Maxime Soki na Verckys Kiamuangana uliosababishwa na kile kinachoelezwa kuwa kundi la “Bela-Bela” likiwa chini ya LEBO (VÉVÉ), Maxime Soki, hajazingatia maelekezo ambayo alipewa na LEBO “VÉVÉ”.
Wanamuziki wa Kundi la “Bella-Bella” walitakiwa kwenda Mjini Lubumbashi kufanya onyesho kutokana na mkataba, lakini badala ya kwenda Lubumbashi, Maxime Soki yeye alichukua usafiri akaondoka na kundi hilo wakaenda kufanya onyesho katika mji wa Matadi.
Kitendo hicho kilimkasirisha sana “Verckys Kiamuangana,” akaamua kumsimamisha kazi kwa muda Maxime Soki. Kitendo hicho kilitafsiriwa kama udhalilishaji, na Maxime Soki na hakukubaliana na uamuzi huo, hivyo akaamua kujiondoa kwenye lebo ya Veve.
Baada ya kufanya uamuzi huo, Maxime Soki alijaribu kumshawishi Nyboma aongozane nae, ila Nyboma alikataa pendekezo hilo. Maxime Soki, akaondoka akiwa na ndugu yake Emile pamoja na mpiga gita Shaba Kahamba.
Mwaka 1973 , Nyboma akaanzisha bendi ya Lipua-Lipua akiwa na Pepe Kalle. Mwaka huo huo wa 1973 akateuliwa Msanii Bora wa Mwaka 1973, na Mwaka 1974, akateuliwa tena kuwa msanii bora.
Nyboma na Pepe Kalle waliamua kuiita bendi yao jina la Lipua Lipua kwa sababu Lipua-Lipua kwanza ni wimbo uliotungwa na “MELEMBU” wakati bado wakiwa katika bendi ya Bella-Bella. Lipua-Lipua ikimaanisha “Wasichana wasiodumu kwenye mahusiano na Mtu mmoja”, leo na huyu, kesho na mwengine.
Kitendo chao cha kutoongozana na Okestra BELLA-BELLA na kuamua kubaki chini ya uongozi wa LEBO “VEVE”, ndicho kilichosababishwa wakapachikwa pia Jina la Lipua-Lipua.
Akiwa na bendi ya Lipua-Lipua, ,Nyboma alitunga nyimbo nyingi, zikiwemo:’ Amba, Mwaluke, Ayidjo, Ditutala, Niki Bue’.
Bendi ya Lipua-Lipua ilikuwa na wanamuziki hawa : Rickos Tonton (Solo Gita), Mulembu (Mwimbaji), Assossa Tshimanga (Mwimbaji), Barly Barliento (Bass Gita), Bisikita Piet (Rhythm Gita), ambae baadae   mpiga rhythm Mombassa Vata, akaja kuchukua nafasi yake.
Jina Lipua-Lipua likaleta shida baada ya bendi hiyo kuamua kujiondoa kwenye lebo ‘Veve’, kitendo ambacho Verckys Kiamuangana hakuridhishwa nacho, akawaomba wabaki chini ya lebo hiyo, ikashindikana. Kuona hivyo, akawazuia kutumia jina Lipua-Lipua akawaeleza kwamba hawana ruksa ya kutumia jina hilo ambalo kwake yeye ni hatimiliki ya LEBO yake (VEVE / SAKUMUNA).

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.