Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Gairo

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Japhari Kubecha, ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilayani humo kwa kazi nzuri ya ukusanyaji mapato ya serikali.
Aidha amesisitiza kwamba juhudi hizo zimechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa rasilimali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akizungumza ofisini kwake baada ya kutembelewa na Meneja wa TRA Wilaya ya Gairo, Ditram Wila, pamoja na Afisa Mwandamizi Elimu na Mawasiliano wa TRA Mkoa wa Morogoro, Immaculate Chaggu, waliofika kumpatia zawadi ya Ushirikiano wa mwaka 2025 kutokana na mshikamano aliouonyesha kwa mamlaka hiyo, DC Kubecha alisema TRA imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wafanyabiashara wanatimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati.
Aidha, alieleza kuwa ushirikiano mzuri kati ya TRA, wafanyabiashara na viongozi wa serikali ni msingi muhimu wa mafanikio katika ukusanyaji wa mapato.

Dar es Salaam

Na Laura Mwakalunde

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi amewataka watawa kufamu kuwa mwaka 2025, ulikuwa wa neema na majonzi.
Askofu Mkuu Ruwa’ichi alisema hayo hivi karibuni wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Nadhiri za Masista wa Shirika la Mtakatifu Fransiko wa Asizi Dada Wadogo, iliyofanyika katika Nyumba Kuu ya Shirika hilo -Mbagala jimboni humo.
“Mwaka 2025 ulikuwa ni mwaka wa neema kwa sababu ndiyo mwaka pekee wa Jubilee Kuu, japo ulikuwa ni mwaka wa majonzi, masikitiko na vifo ila Mungu hakutuacha wala kututupa kwani ndiye tegemeo na kimbilio,”alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.

Dar es Salaam

Na Laura Mwakalunde

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amesema kuwa haki na amani ni vitu viwili vinavyotegemeana, na haviwezi kutenganishwa.
Askofu Mkuu Ruwa’ichi alisema hayo hivi karibuni, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Mkesha wa Noeli, uliofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Yosefu, jimboni humo.
“Amani na haki ni zawadi na ni wasifu unaofungamana na Kristo Mwokozi, kwani Watanzania wengi kwa ujinga na kurubuniwa, wanajidai wao ni wadau wa amani na kusahau kuwa, hakuwezi kuwa na amani bila haki,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.

Bagamoyo

Na Laura Mwakalunde

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, amesema kwamba  vijana wasipotumia vyema mifumo ya mitandao (digitali), itawaharibia maisha yao.
Askofu Mchamungu alitoa wito huo hivi karibuni, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya ufukweni (Beach Mass), iliyofanyika kwenye ufukwe wa Bahari, Jimbo Katoliki la Bagamoyo.
“Mambo yanayowakabili watu wengi na kuwaharibu Wakatoliki ni digitali, ambayo inaweza kuwavuruga na kusababisha kufanya mambo yasipendeza, na yenye chukizo kwa Mungu,” alisema Askofu Mchamungu.
Aidha, aliwataka vijana hao kufahamu kuwa utu wa mtu ni muhimu zaidi katika maisha, na ni vizuri kuthaminiwa kwa sababu ndio zawadi pekee kutoka kwa Mungu.

MAPUTO, Msumbiji
Mwadhama Pietro Kardinali Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican amefanya hija ya kitume nchini Msumbiji kama sehemu ya Maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka 30 tangu Vatican ilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Msumbiji Desemba 14, 1994, miaka 30 iliyopita, sanjari na Jubilei ya Miaka 50 tangu Msumbiji ijipatie uhuru wake wa bendera.
Sambamba na hnayo, katika Ziara yake Kardinali Parolin alikutana pia na kuzungumza na Viongozi Wakuu wa Serikali ya Msumbiji, wakiongozwa na Rais Margarida Adamugy Talapa.

MAPUTO, Msumbiji

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni, Baba Mtakatifu Leo XIV ameunda Jimbo Jipya la Caia (Dioecesis Caiana), nchini Msumbiji, na kumteuwa Askofu Msaidizi António Manuel Bogaio Constantino, M.C.C.J., wa Jimbo Kuu Katoliki la Beira, nchini humo, kuwa Askofu wake wa kwanza.
Jimbo la Caia limeundwa baada ya Baba Mtakatifu Leo XIV kumega Jimbo Kuu Katoliki la Beira, Jimbo Katoliki la Chimoio, Quelimane na Jimbo Katoliki la Tete, huku Jimbo hilo jipya likiwa na Parokia 16, Mapadre wa Jimbo 15, Watawa wa kike 17, na Waseminari 18.
Kwa mujibu wa Vatican News, lengo la Mama Kanisa kuunda Majimbo mapya ndani ya Kanisa Katoliki, kunalenga kusogeza huduma za kiroho na kichungaji kwa watu wa Mungu.

VATICAN CITY, Vatican

Baba Mtakatifu Leo XIV ametuma misaada ya kifedha kwa ajili ya Dominika ya Familia Takatifu ili kusaidia familia zilizoathiriwa zaidi na mabomu ya Nchi ya Ukraine, ambapo umeme, maji na joto havipo.
Mwadhama Konrad Kardinali Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Upendo aliripoti “ubembelezaji mdogo” wa Papa Leo XIV, ambao umesababisha kutoa misaada ya kifedha kutumwa sehemu mbalimbali za dunia kusaidia familia hizo, ambapo Malori matatu ya misaada ya kibinadamu yaliwasili katika maeneo hayo yaliyoathiriwa.

VATICAN CITY, Vatican

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Leo XIV amekutana na kuzungumza na kikundi cha wanahija kutoka Parokia ya Mtakatifu Thomás wa Villanuova - Alcalá ya Henares nchini Hispania.
Katika hotuba yake kwa lugha ya kihispania, Papa alionesha furaha yake kukutana nao katika siku ya Oktava ya Noeli na kuwakaribisha sambamba na kuzungumza nao mambo mbalimbali.
Kama Jumuiya ya Parokia, alisema kwamba waliweza kujiandaa kwa jitihada kubwa katika hija ya kijubilei na wakati wa mwaka huu kwa namna ya pekee kwa Kanisa ambapo walimsindikiza Mfuasi wa Mtume Petro kwa sala zao na kwa ukarimu wao.

Dar es Salaam

Na Dk. Felician B. Kilahama

Mapokeo ya kihistoria tangu miaka ya 1880, yanathibitisha kwamba baadhi ya mataifa barani Ulaya mathalani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ubelgiji na Hispania, yaliweza kufika barani Afrika.
Hivyo, 1884 kukafanyika kikao maalumu jijini Berlin-Ujerumani, kwa lengo mahususi kugawana maeneo kuitawala Afrika.
Kwa upande wa Afrika-Mashariki, Wajerumani wakatawala “Tanganyika” na wakaweza kufika maeneo ya Iringa, ambako Hifadhi-Ruaha inapatikana. Wakiwa huko waliona sehemu imesheheni rasilimali nyingi za wanyamapori, na kuifananisha na “Bustani ya Edeni”.
Kiuhalisia Ruaha kuna urithi wa aina yake, mathalani milima na mabonde pamoja na rasilimali-misitu aina ya miombo, misitu inayostawi kandokando ya mito, na Mto Ruaha-Mkuu. Mto huu ni msaada mkubwa aina yake, ikiwemo wanyamapori wanaoishi kwenye hifadhi ya Ruaha.

Waamini kutoka Parokia mbalimbali za Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Nadhiri za Kwanza za Masista wa Shirika la Mtakatifu Fransisko wa Asizi Dada Wadogo, iliyofanyika katika Makao Makuu ya Shirika hilo, Mbagala-Dar es Salaam.

Page 1 of 60