Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Maaskofu wazindua kampeni kufuta madeni

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Zambia (ZCCB) wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya kuzindua Kampeni ya Kufuta Madeni ya Mwaka wa Jubilei 2025. Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Zambia (ZCCB) wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya kuzindua Kampeni ya Kufuta Madeni ya Mwaka wa Jubilei 2025.

LUSAKA, Zambia

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Zambia (Zambia Conference of Catholic Bishops: ZCCB) limezindua Kampeni ya kufuta madeni ya Mwaka wa Jubilei 2025, ikitoa wito wa msamaha wa haraka wa deni, haki ya kiuchumi, na uwazi katika usimamizi wa madeni ya Zambia.
Uzinduzi huo ulifanyika katika Kapingila House mjini Lusaka nchini humo mwishoni mwa Mkutano wa Kwanza wa Baraza Kuu wa ZCCB kwa 2025, iliyokwenda na wito wa Baba Mtakatifu Fransisko wa haki ya kiuchumi na msamaha wa madeni duniani kote kama sehemu ya Mwaka wa Jubilei 2025.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais wa ZCCB, Askofu Mkuu Ignatius Chama wa Jimbo Kuu Katoliki la Kasama, alisisitiza tena msingi wa Kibiblia wa mapokeo ya Jubilei, akinukuu kitabu cha Mambo ya Walawi, 25:1-8 kinachosisitiza huruma, haki na ufufuaji wa jamii zilizoelemewa na madeni yasiyo ya haki.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.