Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Padri afafanua maana ya Ekaristi

Paroko wa Parokia ya Yohane wa Mungu – Yombo Vituka, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Patrick Bwakila akiwahamasisha Waamini kuchangia ujenzi wa nyumba mpya ya Mpadri, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyokwenda sanjari na kuwapatia watoto Sakramenti ya Ekaristi Takatifu. (Picha na Yohana Kasosi) Paroko wa Parokia ya Yohane wa Mungu – Yombo Vituka, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Patrick Bwakila akiwahamasisha Waamini kuchangia ujenzi wa nyumba mpya ya Mpadri, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyokwenda sanjari na kuwapatia watoto Sakramenti ya Ekaristi Takatifu. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Yohane wa Mungu – Vituka, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Patrick Bwakila amewataka watoto kutokuufananisha mkate uletao uzima (yaani Mwili wa Kristu) na mikate mingine, kwani wanapokula Mkate huo, wanamla Kristu mwenyewe.
Aliyasema hayo wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyokwenda sanjari na kuwapatia watoto hao Sakramenti ya Ekaristi Takatifu katika Parokia ya Yohane wa Mungu – Yombo Vituka, jimboni humo.
“Ndugu zangu wanangu wapendwa, Mama Kanisa alitufundisha kwamba Sakramenti ya Ekaristi Takatifu ni Sakramenti ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristu, Mungu kweli na Mtu katika maumbo ya mkate na divai…
“Kumbe, mkate tunaokula leo, siyo ule wa mama mpika chapati, hapana, ni Kristu mwenyewe ndiye mnayemla leo. Na Kristu mwenyewe anatuambia, aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, huyo hukaa ndani yangu, na mimi hukaa ndani yake. Huu ni mkate wa uzima, mkate uletao uponyaji, afya ya roho, mkate unaotustahilisha sisi huurithi na kupata uzima wa milele,” alisema Padri Bwakila.
Padri Bwakila aliwaonya watoto hao kuepuka kumuasi Kristu mara baada ya kupokea Sakramenti hiyo Takatifu, na kuongeza kwamba atakayefanya hivyo, atatakiwa kuacha kushiriki sakramenti, kwani amemkana na kumkimbia Kristu.
Pia, aliwataka kukumbuka kwamba kwa Sakramenti hiyo ya Ekaristi Takatifu waliyoshiriki katika adhimisho hilo la Misa Takatifu, wametengeneza mahusiano ya kudumu na Yesu Kristu, ambaye ndiye waliyemla.
Mmisionari huyo wa Shirika la Watumishi wa Wagonjwa(Wakamiliani), aliwasihi watoto hao kujitahidi kujibidiisha siku zote, ili watamani na waendelee kupokea chakula hicho ambacho ni kitakatifu.
Aliongeza kwamba haipendezi kwa mtoto ambaye amepokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, na baada ya hapo, haonekani kanisani kushiriki katika Adhimisho la Misa Takatifu.
“Leo umepokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu, baada ya hapo unasema sasa Kanisa ‘bye bye’. Ukifanya hivyo, na Yesu naye atakwambia ‘bye bye’. Utatoroka kanisani, utaliacha kanisa, utaenda kuhangaika, baadaye likikupata tatizo, utaanza kusema ‘Mungu wangu mbona umeniacha,” alisema Padri huyo.
Aliwasisitiza kutokumwacha Mungu ambaye tayari wameshatengeza mahusiano mazuri naye, kwani faida ya kuwa karibu na Mungu wataiona mbinguni.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.