Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Viwanda kuchakata mazao kujengwa

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (mwenye kofia) akizindua Jiwe la Msingi la ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Magonjwa ya Mimea sanjari na kusisitiza ujenzi wa Kongani ya viwanda vya kuchakata mazao ya mikoa ya kusini eneo la Maranje mkoani Mtwara. Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (mwenye kofia) akizindua Jiwe la Msingi la ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Magonjwa ya Mimea sanjari na kusisitiza ujenzi wa Kongani ya viwanda vya kuchakata mazao ya mikoa ya kusini eneo la Maranje mkoani Mtwara.

MTWARA

Na Mwandishi wetu

Serikali imesema kuwa itajenga Kongani ya Viwanda vya kuchakata mazao ya Mikoa ya Kusini kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 300.
Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Mtwara, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, kuwa alisema iwe jua ama mvua itajenga Kongani ya Viwanda vya kuchakata mazao ya Mikoa ya Kusini eneo la Maranje Mkoani Mtwara yenye gharama ya zaidi ya sh. Bilioni 300.
Kongani ya Viwanda (Industrial Park) inajengwa katika kijiji cha Maranje na Tulia, Kata ya Mtiniko, Nanyamba Mji, Mkoani Mtwara
Alisema eneo la mradi lina jumla ya ekari 1,572, ambapo eneo linaloendelezwa kwa sasa ni ekari 354, na ekari 1,218 zilizobaki zitasafishwa na kuwekewa uzio mwezi ujao.
Waziri Bashe alieleza kuwa, Kongani hiyo ya Viwanda ndilo suluhisho la changamoto walizonazo wakulima wa mikoa hiyo.
“Wapo watu walisema ni ndoto, haitawezekana leo, nawaambia Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni msikivu na mtendaji, ameamua iwe jua iwe mvua, Kongani itajengwa hapa na itahusisha viwanda mbali mbali vya kuchakata korosho, ufuta, mbaazi na mengine,”alisema Waziri Bashe.
Alisema, Serikali imeanza hatua za awali za ujenzi wa Kongani hiyo, na zaidi ya sh. Bilioni 7 zimewekezwa.
“Mradi huu mkubwa unaoitwa Dkt Samia Suluhu Hassan, unalenga kujenga viwanda vya kubangua korosho visivyopungua 30 kwa awamu, na tayari zaidi ya shilingi bilioni saba zimetumika kujenga maghala mawili na kisima kimoja,”allisema Bashe.
Aliongeza pia kuwa maghala hayo mawili ya awali, yenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 za korosho, yanatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba mwaka huu, ili msimu wa korosho wa mwaka kesho uanze kwa ufanisi.
alisema huo pia utatoa fursa za ajira kati ya watu 33,000 mpaka 35,000 ambapo ajira za kwanza zitanufaisha wananchi wenyeji .
“Mradi huu unatarajiwa kuajiri kati ya watu 33,000 mpaka watu 35,000 na utakuwa suluhisho la changamoto ya muda mrefu juu ya bei ya korosho kwa mikoa yote inayolima korosho, ikiwemo Mtwara, Ruvuma, na Lindi. Serikali yenu ni sikivu haitarudi nyuma, hiki kiwanda kitajengwa kwa maslahi ya wananchi wa kusini,”alisisitiza Bashe.
Aidha, Waziri Bashe alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kurejeshwa kwa agenda ya ushuru wa mauzo ya nje, lengo ni kuwezesha upatikanaji wa ruzuku na pembejeo, ili kumuinua mkulima.
Bashe alisema kuwa fedha hizo za ushuru huo zikikusanywa, zinarudi Bodi ya Korosho ili kusimamia mahitaji ya korosho.
“Faida zake ni kubwa kwa kuwa ushuru huu sasa unarudi bodi ya Korosho ili kuwezesha wakulima wa zao hilo. Sasa tumetoka kuzalisha tani 180,000 hadi tani 310,000 na tunatarajia kufikia tani 500,000”, alisema.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota alimpongeza Waziri Bashe kwa mapambano ya kutetea maslahi ya wakulima wadogo nchini.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.