Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Rais alishukuru Kanisa kuunga mkono madeni

Bwana Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Zambia alipomtembelea Papa Fransisko Bwana Hakainde Hichilema, Rais wa Jamhuri ya Zambia alipomtembelea Papa Fransisko

LUSAKA, Zambia

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema amelishukuru Kanisa Katoliki nchini humo kwa kuunga mkono juhudi za kurekebisha na kupunguza madeni nchini humo.
Katika ziara ya Balozi wa Vatican katika Makao Makuu ya Rais huyo hivi karibuni, Rais Hichilema alitambua jukumu lililofanywa na Kanisa Katoliki katika kuunga mkono juhudi za kurekebisha deni la Zambia, akibainisha kwamba michango ya Kanisa inaendana na malengo ya Zambia kupunguza madeni na kufufua uchumi.
Hiyo ilifuata katika kushukuru Ujumbe wa 58 wa Amani Duniani wa Baba Mtakatifu Fransisko unaoongozwa na kauli mbiu: “Utusamehe makosa yetu, Utupe Amani.”
Katika fursa hiyo, Rais wa Zambia Bwana Hakainde Hichilema alitaka kutoa heshima wakati wa mkutano wake na Balozi wa Vatican huko Lusaka nchini humo, Askofu Mkuu Gianluca Perici.
Katika mkutano huo, Rais Hichilema alitambua hasa jukumu muhimu lililofanywa na Kanisa Katoliki katika kuunga mkono juhudi za kurekebisha deni la Zambia, huku akibainisha kwamba michango ya Kanisa inaendana na malengo ya Zambia ya kupunguza madeni na kufufua uchumi.
Hiyo ni pamoja na kuunga mkono nafasi ya Zambia katika mfumo wa msamaha wa madeni wa G20, ambapo Rais Hichilema alisisitiza kuwa utawala wake umejitolea kuwekeza kiasi kinachotokana na msamaha wa madeni katika uwekezaji wa kimkakati na ushirikiano wa kibiashara wa kimataifa, ili kukuza maendeleo ya nchi.
Katika hotuba yake, Hichilema alisisitiza dhamira ya Serikali ya kufanya kazi kwa karibu na mashirika ya kidini, hasa Kanisa Katoliki, ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu, afya na ustawi wa jamii nchini Zambia.
Rais huyo alisisitiza kuwa sera shirikishi ya Zambia ya kushirikiana na Mashirika ya Kidini, ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha ustawi wa raia wa nchi hiyo.
Balozi wa Vatican nchini Zambia, Askofu Mkuu Perici aliwasilisha kwa Rais ujumbe maalum kutoka kwa Baba Mtakatifu Fransisko, huku akielezea shukrani kwa juhudi za Zambia katika mchakato wa kurekebisha madeni.
Ujumbe huo, kwa kuzingatia Siku ya 58 ya Amani Duniani, kwa hakika unahimiza ushirikiano kati ya Kanisa na Serikali ya Zambia, na kwamba Baba Mtakatifu Fransisko aliakisi mada za amani, maelewano na msamaha wa madeni, huku akitoa wito wa kuimarisha uhusiano kati ya Vatican na Zambia, na zaidi hata hisia alizoshiriki wakati wa ziara ya Rais Hichilema mjini Vatican mnamo mwaka 2022.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa nchini Zambia, Mulambo Haimbe aliongeza kusema kuwa ujumbe wa Papa Fransisko ni kielelezo cha uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia wa Zambia na Vatican, ambayo itaadhimisha miaka 60 mwaka huu 2025 tangu ulipoanzishwa uhusiano huo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.