Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Msuva kutua Simba na Yanga bado kitendawili

Simon Msuva Simon Msuva

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Simon Msuva amefunguka kuwa hafikirii kurejea nchini kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwa bado anajiona ana uwezo wa kuendelea kupambana katika soka la ushindani nje ya nchi.
Msuva alisema kuwa pamoja na umri wake wa miaka 31, lakini haumfungi yeye kutundika daruga hivi karibuni na kufungua milango ya kurudi kucheza katika Ligi Kuu Tanzania.
Alidai kuwa muda ukifika atarejea nchini, ila kwa sasa bado ana njaa ya kutafuta fedha, na ikitokea amerudi Tanzania basi itakuwa ni mipango tu ya Mungu, ila kwa sasa bado sana kurejea nchini, kwani anatamani kuendelea kusakata kabumbu kwa miaka mingi zaidi nje ya nchi.
Alisema kuwa kwa sasa yeye maamuzi yake ya kuendelea kupambana nje ya nchi ni kuhakikisha anatafuta hela kwa kila hali, kwani bado ana nguvu kuliko vijana ambao kwa sasa wanaonekana wako vizuri uwanjani.
“Itakapofikia, nitarudi tu Tanzania wala Watanzania wasijali, ila kwa sasa bado sana naitafuta hela Waswahili wanasema kwa sasa nina njaa, kwani nataka kuendelea kutafuta hela sana, na wala siyo kurudi nchini kwa sasa”, alisema Msuva.
Alisema kuwa wakati ukifikia, ataweka wazi wazi kuwa ni wapi atakapomalizia soka lake, kama ni Simba au Yanga, ila kwa sasa bado hajafikiria kurudi, kwani mipango yake ni kuendelea kupambana kukusanya sana fedha.
Aidha, aliweka wazi kuwa maamuzi hayo ni ya kwake, na wala siyo ushauri wa mtu mwingine yeyote, kwani anachokifahamu ni kuwa muda bado unamruhusu kuendelea kuonekana sana uwanjani kutokana na uwezo aliokuwa nao.
Msuva alisema kuwa soka lake lazima atalimalizia Tanzania, hivyo kuhusu kuchaguliwa timu ya kucheza pale ambapo atakaporejea, siyo kitu ambacho atakiwekea kipaumbele, kwani anatamani kumaliza soka lake kwa heshima ili historia yake iendelee kuandikwa.
Aliendelea kudai kuwa siyo ndani ya miaka mitatu au minne ya hivi karibuni kurejea nchini, kwani bado ana nguvu za kutafuta hela katika soka la Kimataifa.
“Hayo ni maamuzi yangu mwenyewe, na siyo ya mtu mwingine kunichagulia nikacheze Simba au Yanga, kwani nina nguvu sana ya kukimbia zaidi ya wachezaji wengine vijana. Hivyo, sijachoka kama wengine wanavyodhani”, alisema Msuva.
Msuva ni mmoja ya wachezaji waliofanikiwa kuisaidia Taifa Stars kufuzu kucheza michuano ya Afcon mwaka 2027, na amekuwa msaada mkubwa katika timu hiyo kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa.
Katika misimu ya karibuni, Msuva amekuwa akihusishwa kurudi katika klabu za nyumbani Tanzania lakini mwenyewe amesema bado hajaamua, na Watanzania wasiwe na wasiwasi ni wapi atakapocheza, kwani atahitaji muda wa kufikiria juu ya kucheza Simba au Yanga.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.