Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu anyooshea kidole Watawa wenye mzaha

Mhudumu Mkuu wa Shirika la Dada Wadogo, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Sista Doreen Mwakaliku, akiwakabidhi  nguo baada ya kupandishwa hadhi ya utawa Wapostulanti na kuwa Wanovisi katika Shirika hilo. Mhudumu Mkuu wa Shirika la Dada Wadogo, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Sista Doreen Mwakaliku, akiwakabidhi nguo baada ya kupandishwa hadhi ya utawa Wapostulanti na kuwa Wanovisi katika Shirika hilo.

DAR ES SALAAM

Na Laura Chrispin

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba, amewasihi Watawa kutambua kwamba wito ni zawadi ya thamani kutoka kwa Mungu, hivyo wasifanye mzaha.
Alisema hayo hivi karibuni  wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kupandishwa hadhi ya Utawa kwa Wapostulanti kuwa Wanovisi, iliyofanyika katika Kituo cha Kiroho -Mbagala, jimboni humo.
“Wito ni zawadi ambayo usipoitambua, utaipoteza, na baadaye utajutia, kwani utakuwa umepoteza tunu ya thamani zaidi kwa sababu ya kufuata mikumbo katika jumuiya, kwa kusikiliza maneno ya wengine na kusahau ulichoitiwa na Mungu, kwa sababu ya tamaa ya ulimwengu na uwongo wa watu wa nje,” alisema Askofu Musomba.
Aidha, alisema kuwa kuongoka ni kutoka katika fikra zisizo njema, na kuanza kufikiria mambo yanayofaa na kumpendeza Mungu, kwani hata Mtume Paulo aliyekuwa akiitwa Sauli, alikuwa ni mtu aliyewachukia Wakristo, na aliwatesa.
Na hata wakati mwingine alidiriki kuyabomoa makanisa, na hata alipokuwa njiani akielekea Damaskasi nchini Syria kuwatafuta Wakristo, ajabu alisikia sauti ikimwita ‘Sauli Sauli, mbona unanitesa’ na yeye hakutambua ni nani, na sauti imetokea wapi.
Aliendelea kusema kuwa ile sauti ilimjibu na kumwambia, Mimi ni Yesu; na baada ya kuingia Damaskasi, alibatizwa na kupewa maelekezo ya kulijenga Kanisa na kubadilishwa jina na kuitwa Paulo, badala ya Sauli.
Askofu Musomba aliwasihi Watawa wote kupenda kujitoa zaidi kwa kuwatumikia wengine kwa unyenyekevu mkubwa, bila kujibakiza wala kujali chochote au kusema wanaonewa na wengine au kuteswa, badala yake wanatakiwa kutambua wapo kwa ajili ya kutumwa, kwani waiitwa na wakaitika.
Askofu Musomba alisema umoja na upendo unaweza kuharibika kwa sababu ya udanganyifu na hisia, na kuwasihi kuwakemea Watawa wengine ambao watakuwa wanaenda tofauti na mapenzi ya Mungu, na kuwataka watambue wakifanya hivyo itawafanya waishi vizuri zaidi.
Aliendelea kusema kuwa Mungu hapendi kuona jumuiya yenye magomvi na masimango, wala kuona jumuiya ya watu wenye roho mbaya, badala yake wanatakiwa kutengeneza jumuiya yenye upendo na upatanisho.
Askofu Musomba aliwapongeza Wapostulanti watano kwa kuvuka hatua na kuwa Wanovisi, na kuwataka wawe ni watu wenye unyenyekevu na furaha kama ya wakati ule walipoandika barua ya kuomba kujiunga katika shirika, na kusikia wamekubaliwa ombi lao.
Askofu Musomba alisema kwamba ukiona mwenzako anafanya vibaya, alafu unampongeza na kufurahia ujue hiyo ni tabia mbaya, na kuwaasa wasidanganyike katika safari yao ya Utume bali wazidi kumwomba Mungu ili wazidi kukua kiimani.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.