Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu: Waamini acheni uchochezi

Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu – Buza, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakitoka kanisani baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ilyoadhimishwa hivi karibuni na Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Mhashamu Stephano Musomba (hayupo pichani). (Picha na Yohana Kasosi) Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu – Buza, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakitoka kanisani baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ilyoadhimishwa hivi karibuni na Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Mhashamu Stephano Musomba (hayupo pichani). (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Waamini wamekumbushwa kuwalinda, kuwatunza, na kuwapenda Mapadri wao, na kamwe wasikubali Mapadri wao wachafuliwe na mtu mmoja au kikundi cha watu.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba alitoa wito huo hivi karibuni wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, alipofanya ziara yake ya kichungaji katika Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu – Buza, jijini Dar es Salaam.
“Sasa niwaombe kitu kimoja, endeleeni na ukarimu huo. Wapendeni Mapadri wenu, nafahamu kwamba mna Mapadri wawili hapa, jitahidini kuwapenda na kuwalinda, wetendeeni mema Mapadri wenu, msikubali Mapadri wenu wapate changamoto, msikubali Mapadri wenu wachafuliwe na mtu mmoja au kikundi cha watu, hakikisheni mnaendeleza ushirikiano kati yenu na Mapadri wenu katika Parokia hii ya Buza,” alisema Askofu Musomba.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.