Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Wabunge wamhofia Mkandarasi Ujenzi Uwanja wa Ndege Msalato

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (mwenye kipaza sauti), akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea ujenzi wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (mwenye kipaza sauti), akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea ujenzi wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato.

Dodoma

Na Mwandishi wetu

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeshauri Serikali kusimamia vyema Mkandarasi anayejenga uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato jijini Dodoma ili akamilishe ujenzi huo kwa wakati.
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso alisema kuwa ni vema mkandarasi akaharakisha ujenzi wa uwanja huo, ili kwenda na mkataba wa ujenzi.
Alifafanua kwamba kumekuwa na tabia kwa baadhi ya Wakandarasi kuomba kuongezewa muda wa ziada wanapopewa kazi, bila kujua muda utakapoongezwa na gharama nazo zinaongezeka.
Hivyo wao kama Kamati, wanashauri Serikali kwanza ni kumsimamia mkandarasi akamilishe ujenzi kwa wakati.
“Kumekuwa na tabia ya Wakandarasi wetu wanapopewa kazi wanaongeza muda wa ziada ambao hautakiwi uingezwa mara kwa mara, Hivyo tunaomba eneo hili Serikali isimamie, kwani anapoongezewa muda, na gharama zinazidi zaidi za ule mkataba uliokuwa umesainiwa,”alisema kiongozi.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.