Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu Ruwa’ichi: Kwaya si kutumbuiza ni Kuinjilisha

Viongozi wa Kwaya Shirikisho ya Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (UKWAKATA) wakiwashukuru Maaskofu, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi na Askofu wa Jimbo Teule la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Musomba, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya UKWAKATA, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Petro-Oyesterbay, Jimboni humo. (Picha na Yohana Kasosi) Viongozi wa Kwaya Shirikisho ya Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam (UKWAKATA) wakiwashukuru Maaskofu, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi na Askofu wa Jimbo Teule la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Musomba, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya UKWAKATA, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Petro-Oyesterbay, Jimboni humo. (Picha na Yohana Kasosi)

Dar es Salaam

Na Laura Mwakalunde

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddeaus Ruwa’ichi amewataka Wanakwaya kutambua kwamba wanapoimba muziki Mtakatifu,  wazo sio kutumbuiza bali ni kuinjilisha.
Rai hiyo aliitoa hivi karibuni katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania (UKWAKATA), Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Petro-Oysterbay, jimboni humo.
“Wanakwaya siyo watumbuizaji na kama unataka kutumbuiza, basi ni vyema kwenda kwenye mahall ya disco… lakini ukitaka kuinjilisha kwa kuishi ukristo wako na katika kanisa lako, huku ukimshukuru Mungu kwa zawadi ya kipaji alichokujalia cha kuinjilisha kwa njia ya kuimba, salia Kanisani,”alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.
Aidha, alisema kuwa kila mbatizwa anaitwa kuwa shahidi wa Kristo kwa kutumia Kipaji alichojaliwa na Mungu, akiwaasa Wanaukwakata hao, kutumia vyema vipawa vyao.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.