Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Taifa Stars yatisha ugenini kwa dakika 630

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu

Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars imejiwekea rekodi yake binafsi ya kushinda mechi nyingi za kimashindano za ugenini katika kipindi cha mwaka 2016 hadi sasa.
Katika kipindi chote hicho, Stars imeshinda katika dakika 90 za mechi saba za ugenini za mashindano mbalimbali zikiwemo za kuwania kufuzu AFCON (Mataifa ya Afrika), CHAN (Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani), kuwania kufuzu Kombe la Dunia na mashindano yenyewe ya CHAN.
Kwenye mechi za kuwania kufuzu fainali za CHAN na fainali zenyewe, Stars ilifanikiwa kupata ushindi muhimu ugenini ambapo Oktoba mwaka 2019 ilicheza mechi ya kufuzu CHAN ilipindua matokeo ugenini kwa kuichapa Sudan 2-1 na kufuzu mashindano hayo.
Julai 23, 2022, Stars ilicheza mechi ya kufuzu CHAN dhidi ya Somalia na kupata ushindi wa 1-0 ambapo kikanuni Somalia walitumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kama uwanja wao wa nyumbani, na Stars ikashinda ikiwa kama timu ya ugenini.
Agosti 6, 2025, Stars ilipata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Mauritania katika hatua ya makundi ya michuano ya CHAN.
Kwa upande wa mechi za kuwania kufuzu AFCON, Stars iliichapa Guinea 2-1 Septemba 10, 2024 ambapo ilikuwa mechi ya kusisimua ya kuwania kufuzu AFCON 2025 iliyochezwa Yamoussoukro, Ivory Coast, ambapo Stars ilitoka nyuma na kushinda kwa mabao ya Feisal Salum na Bakari Mwamnyeto.
Juni 11, 2024 iliichapa Zambia 1-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la dunia 2026, ushindi uliopatikana kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia, bao likifungwa na Waziri Junior.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.