manchester, Uingereza
Mahakama imeelezwa kuwa bondia na bingwa wa zamani wa dunia, Liam Smith, anadaiwa kumpiga ngumi kichwani mwanaume mmoja wakati mtu huyo akiwa amelala sakafuni na asiye na uwezo wa kusimama.
Smith, ambaye alishikilia taji la WBO la uzani wa ‘light-middleweight’ kuanzia mwaka 2015 hadi 2016, alifika kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Crown ya Manchester kujibu shtaka la kusababisha madhara makubwa ya kimwili kwa makusudi.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 38, kutoka Liverpool, hakutakiwa kutoa majibu (kukiri au kukataa) kuhusiana na shtaka hilo, lililotokana na kukamatwa kwake kwa madai ya kumshambulia mfanyakazi wa mapokezi katika jengo la The Blade, lililopo Silvercroft Street, Deansgate, mnamo Septemba 13.
Mahakama ilielezwa kuwa mtu anayedaiwa kushambuliwa, Laurent Nke, alipata majeraha usoni na kulazwa hospitalini.
Katika kikao kifupi cha mahakama, Jaji Tom Gilbart alibainisha kuwa tukio hilo lilinaswa na kamera za usalama (CCTV).











