Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Shinyanga

Na Angela Kibwana

Mhashamu Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, amewata Wakatoliki kuendelea kuombea na kulinda amani ya nchi, hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano Oktoba 29 mwaka huu, ili uwe huru na haki.
Askofu Sangu alisema hayo, wakati akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu, iliyofanyika Parokia ya Mt. Rosa wa Lima – Kitangili jimboni humo, akiwakumbusha Wakatoliki kumuomba Mama Bikira Maria, alinde familia zao na Taifa kwa ujumla kuelekea Uchaguzi Mkuu, kabla na baada ya uchaguzi huo.

Visiga

Na Laura Mwakalunde

Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Padri Edward Sabbas amesema kwamba, Taifa linaloshindwa kufuata misingi bora ya utu hupotoka.
Padri Edward alisema hayo hivi karibuni, wakati akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Mahafari ya Kidato cha Nne, katika Seminari Ndogo ya Maria –Visiga, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Dar es Salaam

Na Mwandishi Maalumu

Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara, hasa magonjwa yasiyo ambukiza, ili kuepuka madhara zaidi.
Rai hiyo ilitolea hivi karibuni, na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, jijini Dar es Salaam, Dk. Kezia Tessua, wakati akizungumza na Wananchi katika eneo la Bunju, kwenye Programu ya Viongozi Wanawake, inayosimamiwa na Taasisi ya Uongozi.

Dar es Salaam

Na Celina Matuja

Wanafunzi wanaohitimu masomo yao ya Sekondari, katika Shule ya Msingi na Sekondari ya St. Rosalia Kinyerezi, jijini Dar es Salaam, wanapaswa kuangalia fursa za kusomea ubaharia, kwani ni taaluma inayoweza kuwasaidia maishani.
Wito huo ulitolewa na CPA Pascal Karomba, Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), wakati akizungumza katika mahafali ya shule hizo, kwa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari, ili wapate elimu hiyo nzuri ya ubaharia.
Aidha, Karomba aliupongeza uongozi wa shule hizo, kwa kuiona kiu ya Watanzania juu ya elimu, kuondoa ujinga kwa watoto wa kitanzania.

Dar es Salaam

Na Laura Mwakalunde

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amewaonya Waamini kuacha kuwa Wakristo goigoi.
Aliyasema hayo hivi karibuni, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, iliyofanyika Parokia ya Bikira Maria wa Fatima-Msimbazi, jimboni humo.

Mahenge

Na Mathayo Kijazi

Askofu wa Jimbo Katoliki la Mahenge, Mhashamu Agapiti Ndorobo, amesema kuwa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ni vyema kuchagua kiongozi anayefaa na anayejali kila mmoja, bila kuangalia dini, rangi, kabila, wala utaifa wake.
Askofu Ndorobo aliyasema hayo hivi karibuni, wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 75, ya Seminari ya Mtakatifu Francis – Kasita, jimboni humo.

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Imeelezwa kuwa imani ya kweli si kujisifia, kujivuna, wala kujiona, bali kujishusha.
Hayo yalisemwa na Monsinyori Novatus Mrighwa, Mwalimu wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga – Segerea, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara, katika Parokia ya Mtakatifu Gaudance - Makoka, jimboni humo.

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Parokia ya Mtakatifu Peter Claver – Mbezi Louis, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, imeadhimisha Jubilei ya Miaka 25, huku Waamini wakiaswa kuepuka dhuluma, kutafuta ukubwa, umaarufu na kutambulika katika jamii.
Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei hiyo, alisema kwamba:
“Hayo ni mahangaiko makubwa ya wanadamu, kupambana kupata ukuu, kupambana kupata umaarufu, kupambana kuwapiku wengine. Na katika kupambana huko, tunaweza tukatendeana visivyo, tukadhulumiana, tukakanyagana, tunaweza tukakuta mtu anatembea juu ya mabega na vichwa vya wengine ili aonekane, atambulike, aheshimike. Ukuu wa kweli hauji kwa kuwapiku wengine, ukuu wa kweli hauji kwa kuwakanyaga wengine,” alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.

Dar es Salaam

Na Remigius Mmavele

Alain Yoka Mpela almaarufu Afande, alikuwa akiishi na wazazi wake Manispaa ya Matete Jijini Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Akiwa likizo siku moja Baba yake alimtuma kwenda Manispaa ya Bandalungwa kupeleka barua kwa rafiki yake, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni kubwa.
Baada ya kupeleka barua, kwa kuwa mama yake mdogo alikuwa akiishi pia Bandalungwa, ambayo wanaifupisha na kuiita Bandal, aliamua kumtembelea badala ya kurudi nyumbani kwao moja kwa moja. Alipofika nyumbani kwake hakumkuta, hivyo akaanza kucheza mchezo wa “dames”  wakati akimsubiri.
Alipokuwa akicheza, alikuwa akiimba wimbo Abissina wa King Kester Emeneya. Kwa bahati nzuri, Werrason alipita karibu na eneo ambalo Alain Mpela alikuwa anacheza, akasikia sauti ya Alain Mpela akiimba.
Akashangaa na akauliza ni nani huyu kijana, mwenye sauti nzuri tena ya kipekee. Werrason akaenda hadi nyumbani kwa mama mdogo wa Alain Mpela kumsikiliza.

Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

Katika hali ya mateso na mahangaiko ya muda mrefu, kwa baadhi ya Mataifa ya Afrika, ambayo yalitumbukia kwenye mikono ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, sasa mataifa mengi yameanza kutaka kujinasua kwenye mikono ya vita na vurugu za hapa na pale.
Kwa sasa dunia inashuhudia hali mbaya ya vita na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, katika Mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan Kusini na Sudan, bila kusahau huko Gaza ukanda wa Mashariki ya Kati.

Page 1 of 54