Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Morogoro

Na Dk. Felician B. Kilahama

Mwenyezi Mungu aliumba kwa umakini mkubwa sana vyote viijazavyo dunia, ikiwemo misitu na mimea ya aina mbalimbali, na akauweka ulimwengu katika misingi imara isiyotikisika. Imeandikwa katika Biblia Takatifu Kitabu cha Mwanzo, Neno lake Mwenyezi Mungu linaeleza bayana kwamba:
“Mungu akasema nchi na itoe majani/nyasi, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambayo mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi, ikawa hivyo” (Mwanzo 1:11).
Aidha, vyote tunavyovishuhudia kuwepo katika ulimwengu, Mungu alivikamilisha ndani ya siku sita, na siku ya saba akapumzika baada ya kuona kila kitu kimekaa sawa.
Lakini Mwenyezi Mungu, alihitimisha yote kwa kumuumba binadamu kwa sura na mfano wake, mwanaume na mwanamke aliwaumba.

Mwanza

Na Paul Mabuga

Katika harakati za kutafuta maisha kwa vijana kumekuwa na changamoto nyingi, wanazopitia, kwenye michakato yao ya kusaka maisha bora.
Miongoni mwa vijana ambao wamesaka maisha ni Anna Nicodemus, mmoja wa Wahariri katika kituo cha runinga, cha Shirika la Utangazaji la Namibia [NBC].
Yeye na timu yake walipanga kufanya filamu halisi [factual film], kama sehemu ya mafunzo ya chuo kimoja katika Jiji la Berlin, nchini Ujerumani. Na wameamua kuifanya kazi hii katika nchi yao.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi akiwa katika picha ya pamoja na Wanajubilei wa Miaka 50 na 25 ya Upadri, Mapadri na Mashemasi baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya shukrani, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Msimbazi Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. (Picha zote na Yohana Kasosi)

Maaskofu wa Majimbo mbalimbali ya Kanisa Katoliki Tanzania wakiwa katika Adhimiso la Misa Takatifu ya kumuombea Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa katika Kanisa Kuu la Maria Mama wa Huruma Jimbo Katoliki Bukoba.

Maaskofu kutoka Majimbo mbalimbali ya Kanisa Katoliki Tanzania wakiwa katika maandamano kuingia kanisani kuadhimisha Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 100 ya Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo - Kipalapala, Jimbo Kuu Katoliki la Tabora. (Na Mpigapicha wetu)

VATICAN CITY, Vatican

na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher amesisitiza ukweli wa dharura wa hatari zinazozunguka maendeleo ya Akili Unde katika uwanja wa kijeshi, na kusema kuwa Teknolojia haipaswi kuchukua nafasi ya hukumu ya binadamu katika masuala ya maisha na kifo.
Askofu Mkuu Gallagher alisema hayo katika mjadala wa wazi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huko New York, nchini Marekani, ambapo alisisitiza kuwa wito wa Vatican ni kusitishwa mara moja kwa silaha hatari zinazojiendesha, na kusema kwamba ni hatari kutumia AI katika mifumo ya amri na udhibiti wa nyuklia.

VATICAN CITY, Vatican

Hivi karibuni Padri Petro Paolo Oros, Mfiadini wa utawala wa Kikomunisti, aliyeuawa mwaka 1953 akiwa na umri wa miaka 36, ametangazwa kuwa Mwenyeheri.
Katika kutangazwa Mwenyeheri Padre huyo huko Bilky nchini Ukraine, Mwadhama Grzegorz Kardinali Ryś, Askofu Mkuu wa Łódź, nchini Poland, na Mwakilishi wa Papa, alisema kwamba katika dunia ya leo iliyosambaratishwa na vita vya kutisha, vilivyogawanyika zaidi ya hapo awali, na ambapo ubinadamu umepoteza uwezo wa kukutana kwa kina na unakabiliwa na upweke wa kutisha, Kanisa linahitaji watu wa kukutana na ushirika wa kweli, kama alivyokuwa Petro Paolo Oros.

Lilongwe, Malawi

Baraza la Maaskofu Katoliki Malawi (Malawi Conference of Catholic Bishops: MCCB) limempongeza Profesa Arthur Peter Mutharika kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa saba wa Jamhuri ya Malawi.
Katika taarifa iliyotiwa saini na Rais wa MCCB, Askofu Martin Anwel Mtumbuka alitoa pongezi za dhati kwa mkutano huo kwa Profesa Mutharika kwa ushindi wake katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni.

SOLWEZI, Zambia

Katika Mkutano Mkuu wa 14 wa Baraza la Maaskofu wa Kusini mwa Afrika (IMBISA) katika Jimbo Katoliki la Manzini, Eswatini, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabaraza ya Maaskofu Wanachama Afrika Mashariki (AMECEA), Askofu Charles Sampa Kasonde wa Jimbo Katoliki la Solwezi nchini Zambia, ameshiriki ujumbe wa mshikamano na wajumbe hao, akitaka kuwepo kwa mfumo wa kichungaji unaoathiri masuala mawili ya Kanda.

Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddeus Ruwa’ichi, amewataka Waamini kutoruhusu kugubikwa na huzuni iliyopitiliza pale msiba unapotokea, badala yake waweke imani na tumaini katika Kristo, liwafariji.
Askofu Mkuu huyo alisema hayo wakati wa homilia yake, katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kumwombea Balozi wa Baba Mtakatifu, Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, jimboni humo.