Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

‘Mateso ya watu ni dhambi zao’

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu (wa pili kulia), akikagua ujenzi wa kanisa katika Kigango cha Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu, Parokia ya Mtakatifu Augustino, Salasala jimboni humo, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu. Nyuma ya Askofu ni Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Boniface Ngowi. Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu (wa pili kulia), akikagua ujenzi wa kanisa katika Kigango cha Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu, Parokia ya Mtakatifu Augustino, Salasala jimboni humo, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu. Nyuma ya Askofu ni Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Boniface Ngowi.

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu amesema kuwa dhambi ni hali inayoleta maafa na mateso makubwa kwa watu, kwani ni chukizo kwa Mungu.
Askofu Mchamungu alisema hayo wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu iliyofanyika katika Kigango cha Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Salasala, Parokia ya Mtakatifu Agostino, Salasalaa.
“Dhambi, ndugu zangu ni chukuzi kwa Mungu, kwani dhambi inaleta maafa hata ukiangalia katika Biblia, Mungu aliruhusu watu wake wapelekwe utumwani Babeli…
Ni kwa sabababu ya matokeo ya dhambi, watu hawakumsikiliza Mungu, na matokeo yake ni kupata maafa, na hivyo nasi tujiepushe na dhambi,”alisema Askofu Mchamungu.
Askofu Mchamungu alibainisha kuwa dhambi inaleta madhara kwake mtu binafsi, kwani hata mtu anayeiba anakamatwa, anafungwa, na huko atateseka na kuwa na mahangaiko makubwa kutokana na dhambi aliyotenda.
Askofu huyo aliendelea kufafanua kwamba hata mtu aliyetoa uhai wa mtu mwenzake, anafungwa, na tena kifungo ambacho ni cha maisha, ama kupokea hukumu ya kifo kwa kunyongwa. Hiyo yote ni matokeo ya dhambi, hivyo akiwasihi waamini kukaa mbali na dhambi.
Aonya kuhusu nyumba ndogo:
Kwa mujibu wa Askofu Mchamungu, tabia ya baadhi ya watu kuwa na nyumba ndogo ni dhambi ambayo inatesa wengi, hasa kwa kushindwa kuheshimu ndoa zao, na hivyo kupata mahangaiko ya kutunza familia mbili, ikiwemo isiyo halali, akiwataka waamini kuacha kufanya hivyo.
“Na sisi dhambi tunazozitenda zinatuletea mahangaiko makubwa na mateso, na ukitaka kuishi kwa amani bila mahangaiko mengi, fuata mpango wa Mungu. Endeeleeni kumuamini Kristo, kwani kwa kufanya hivyo, mtapata uzima wa milele,” alisema Askofu Mchamungu.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Agostino, Salasala, Padri Peter Assenga, alisema kuwa uongozi wake kwa kushirikiana na Kamati Tendaji wamefanya jitihada mbalimbali, ikiwemo za kuwahamasisha waamini kushikamana ili kukusanya fedha za kutekeleza ujenzi wa kanisa la Kigango.
Padri Assenga aliitaka Kamati Tendaji kuhakikisha inatekeleza vyema wajibu wake ili kufanikisha mipango waliyojiwekeza ya kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo.
Naye Boniface Ngowi, Mwenyekiti Parokia ya Mtakatifu Augustino, Salasala, alimshukuru Askofu Mchamungu kwa kusali nao katika Misa hiyo na kushuhudia maendeleo ya Kigango hicho chenye historia ya kuwa Parokia hivi karibuni.
Alisema kuwa tangu mwaka 2015 Padri Assenga alipoingia Parokia ya Salasala, alifanya kazi kubwa ya kuanzisha Vigago vya Mtakatifu Sesilia, Kinzudi, na Mtakatifu Dominiko, Mbezi Juu, ambavyo sasa ni Parokia, na Vigango vya IPTL na vingine vingi, kwani ni kazi iliyotukuka.
Ngowi alibainisha kuwa mambo yote yanayoonekana kwa sasa ni matunda ya utendaji mzuri wa Padri Assenga kwa kushikamana na Kamati Tendaji ya Parokia, kwani amefanya mambo mengi parokiani hapo, ikiwemo ujenzi wa kanisa jipya kubwa na zuri.
Aidha, aliwataka waamini wa Parokia ya Salasala kuendelea kushikamana, kwani mafanikio yote yanaletwa na wao waamini wenyewe.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.